Katika Baraza la Madiwani lililofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa Tabora mnamo tarehe 23/02/2018 Mkuu wa Wilaya ya
Tabora Mjini alikabidhi mikopo yenye thamani ya Shilingi milioni thelathini na nne(Tsh milioni 34) kwa vikundi vya kiuchumi vya wanawake na vijana ambapo
vikundi vya wanawake vilipewa Tsh milioni 22, vikundi vya wanawake walemavu vilipewa Tsh milioni 2 pamoja na vikundi vya vijana vilipewa Tsh
milioni 10.
Halmashauri ya manispaa ya Tabora kupitia Idara ya Maendeleo ya jamii kwa kufuata mwongozo wa utoaji wa mikopo kwa wanawake na vijana hutoa mikopo kwa walengwa kupitia fedha zake za makusanyo ya mapato ya ndani kwa kutoa asilimia 10 ya fedha zinazopelekwa kwenye miradi ya maendeleo
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Manispaa Tabora, 4 Barabara ya Kiwanja cha Ndege
Anwani ya Posta: S.L.P 174, 45182 Tabora
Simu ya Ofisi: +255 262606088
Simu ya Mkononi: +255
Barua Pepe: md@taboramc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.