UTANGULIZI.
Idara ya Maendeleo ya Jamii ni miongoni mwa Idara 13 katika Halmashauri ya Wilaya ya Manispaa Tabora. Idara ina jumla ya watumishi 16 wakiwemo Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mafundi sanifu. Halmashauri ya Manispaa Tabora ina kata 29 lakini kata 6 tu ndio zina Maafisa Maendeleo ya Jamii.
Idara ya maendeleo ya jamii inatoa huduma kwa jamii kwa kutumia mbinu shirikishi jamii katika kuwawezesha wananchi kujiletea maendeleo yao wenyewe kwa kutumia rasilimali zilizopo ndani na nje ya jamii. Idara hii inashirikiana na idara zote zilizopo Halmashauri na wadau wote wa maendeleo, makundi mbalimbali katika jamii yakiwemo vijana, watoto, walemavu, wazee, na wanawake katika kufanya shughuli za kijamii na kiuchumi ili mabadiliko chanya na endelevu kwa jamii. Aidha inawezesha kuhamasisha, kuelimisha na ushauri mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuratibu mikopo ya Mfuko wa Maendeleo Wanawake (WDF) na mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF) inayotolewa na Halmashauri ili kuwawezesha wanawake na vijana kiuchumi.
SHUGHULI ZA IDARA.
URATIBU WA MFUKO WA MAENDELEO YA WANAWAKE NA MFUKO WA MAENDELEO YA VIJANA.
MFUKO WA MAENDELEO YA WANAWAKE
Idara ya Maendeleo ya Jamii inaratibu mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) kwa kutoa mikopo kwa vikundi vya kiuchumi vya wanawake. Lengo la mfuko ni kutoa mikopo kwa wanawake ili kuwahimarisha kiuchumi.
2.2. Madhumuni ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake.
Kutoa Mikopo yenye masharti nafuu kwa wanawake wenye kipato kidogo ili kuwawezesha kujiendeleza kiuchumi na hivyo kuinua hali za familia zao.
Kuwa kama mfuko wa dhamana.
Kuongeza ajira na kipato kwa wanawake katika sekta isiyo rasmi.
Kujenga tabia ya kujiwekea akiba kwa ajili ya upanuzi wa shughuli zao na dharula.
Kutafuta vyanzo vya fedha.
2.3. Masharti kupata mkopo wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake;-
Wanawake 5 wenye akili timamu wanaoaminiana, kuelewana, na wawetayari kudhaminiana,
Wasitoke katika kaya/ familia moja.
Kikundi kinatakiwa kuwa na akaunti ya pamoja,
Wanakikundi lazima wachaguane wenyewe kufuatana ma mipango na mahitaji yao,
Lazima waaandike barua ya mkopo pamoja na mchanganuo wa shughuli watakazozifanya.
Barua ya maombi ya Mkopo yapitie kwa Mtendaji wa Kata husika.
Vikundi vilivyonufaika kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake.
Kupitia mfuko wa Maendeleo ya Wanawake, jumla ya vikundi 73 vimepewa mkopo wenye thamani ya Tsh. 49,000,000/- kuanzia mwaka 2013/14 hadi 2016/17. Kwa mchanganuo ufuatao;-
Na.
|
Mwaka
|
Idadi ya Vikundi
|
Idadi ya wanakikundi
|
Kiasi cha pesa(Tsh.)
|
1
|
2013/2014
|
9
|
45
|
5,500,000/-
|
2
|
2014/2015
|
12
|
60
|
7,500,000/-
|
3
|
2015/2016
|
15
|
75
|
11,000,000/-
|
4
|
2016/2017
|
38
|
190
|
25,000,000/-
|
MFUKO WA MAENDELEO YA VIJANA.
Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ulianzishwa na Serikali kwa lengo la kuwasaidia vijana kupata mikopo yenye masharti nafuu na kuwajengea uwezo kiuchumi ili waweze kuanzisha au kuimarisha miradi yao kwa lengo la kujitegemea na kukuza uchumi wa nchi.
Walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ni vijana wote watanzania wanawake na wanaume wenye umri kati ya miaka 18 mpaka 35.
Masharti kupata mkopo wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Awe kijana mwenye umri wa miaka 18 mpaka 35.
Awe na mradi.
Awe katika kikundi cha kati ya wanakikundi 5 mpaka 30.
Wawe na andiko la mradi.
Barua ya andiko la mradi.
Barua ya maombi ya mkopo yapitie kwa Mtendaji wa Kata husika.
Vikundi vilivyonufaika kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Kupitia mfuko wa Maendeleo ya Vijana, jumla ya vikundi 26 vimepewa mkopo wenye thamani ya Tsh. 34 ,000,000/- kuanzia mwaka 2014/15 hadi 2016/17. Kwa mchanganuo ufuatao;-
Na.
|
Mwaka
|
Idadi ya Vikundi
|
Idadi ya wanakikundi
|
Kiasi cha pesa(Tsh.)
|
1
|
2014/2015
|
5
|
85
|
5,000,000/-
|
2
|
2015/2016
|
5
|
90
|
5,000,000/-
|
3
|
2016/2017
|
16
|
153
|
24,000,000/-
|
URATIBU WA SHUGHULI ZA MAPAMBANO DHIDI YA VVU/ UKIMWI.
Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ni miongoni mwa watekelezaji wa juhudi za kupambana na ugonjwa hatari wa UKIMWI kwa kufanya shughuli mbalimbali ambazo zinapelekea kupunguza athari za ugonjwa huu ambao umesababisha madhara makubwa katika nchi yetu. Madhara hayo;- ni kuongezeka kwa idadi kubwa ya Wajane, Wagane, watoto yatima, watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi, kupoteza wataalamu katika fani mbalimbali na hatimaye kupungua nguvu kazi ya Taifa.
Maeneo ambayo idara ya Maendeleo ya Jamii imejikita zaidi ni:
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Manispaa Tabora, 4 Barabara ya Kiwanja cha Ndege
Anwani ya Posta: S.L.P 174, 45182 Tabora
Simu ya Ofisi: +255 262606088
Simu ya Mkononi: +255
Barua Pepe: md@taboramc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.